TAMASHA LA FILAMU LA DAR FILAMU FESTIVAL (DFF 2013)
KUFANYIKA 24TH – 26TH SEPTEMBER 2013 VIWANJA VYA CoICT-
UDSM- POSTA KIJITONYAMA, DAR ES SALAAM.
Kampuni ya Haak
Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa www.filamucentral.co.tz inapenda
kutambulisha kwenu Tamasha la filamu linaloitwa Dar Filamu Festival (DFF) 2013 litalofanyika katika uwanja wa
CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, kuanzia
tarehe 24- hadi 26, September,2013 Tamasha litaambatana utoaji wa Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za
kitanzania kwa watu wote bure kwa siku tatu.Kutakua na filamu nne kwa siku
kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.
Tamasha hilo
limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania na zile
zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa ya ajili kwa vijana na
jamii husika kwa ujumla, filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na
hapa nchini katika kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao
ikiwa kampeni ya filamucentral kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu
Ulimwenguni.
Kwa tamasha hili
la awali tutaonyesha filamu za hapa Tanzania pekee ikiwa ni utambulisho wa Dar
Filamu Festival kwa mara ya kwanza kwenu wanahabari, miaka ijayo Tamasha
litahakikisha linashirikisha filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha
ya Kiswahili kutoka popote Ulimwenguni.
Akiongea na
Waandishi wa Habari mratibu wa Tamasha hilo Staford Kihore pia amesema kuwa
katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu siku tatu hizo kila siku
imepewa jina kwa filamu zitakazoonyeshwa Tarehe 24th September, 2013
siku ya Jumanne ambayo ndio siku ya ufunguzi utakuwa ni usiku wa Bongo Movie
Classics, 25th September, 2013 ni usiku wa Quality Nights.
Na ile siku ya
mwisho tarehe 26th September, 2013 itakuwa ni Stars Nights siku
ambayo kutakuwa na wasanii wetu mbalimbali ambao wanajenga soko hilo la Bongo
movie filamu, Tamasha hili linapambwa na wasanii wote wakiwakilishwa na wasanii
wenzao wawili ambao ni Vincent Kigosi ‘Ray’ kama Official Producer and
Director for DFF 2013 na Elizabeth
Michael ‘Lulu’ kama Official Actress for DFF 2013.
Pia tamasha
litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu kwa asubuhi ambapo madarasa
yataendeshwa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Idara ya Sanaa tarehe 24 September, 2013 masomo ya Uandishi wa Muswada,
Uigizaji na Uongozaji wa filamu
yatafundishwa kwa washiriki, 25th September 2013 Siku nzima Makapuni
ya Utengenezaji filamu yataonyesha na kutangaza kazi zao kwa wadau mbaliambali.
Tarehe 26th
September 2013 ni siku muhimu sana kwani Taasisi kama vile TRA, Bodi ya Ukaguzi
wa filamu na michezo ya kuigiza, Wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine
watakutana katika jukwaa la majadiliano kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu,
pia filamu kadhaa zitaonyeshwa na kujadiliwa na wadau watakaokuwepo matukio
yote ya asubuhi yatafanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa.
Pia tunatoa
shukrani kwa taasisi za Serikali kutuunga mkono katika ufanikishaji wa tamasha
hilli la Dar Filamu Festival (DFF) 2013,
taasisi kama Bodi ya Filamu na ukaguzi wa michezo ya kuigiza Tanzania,
Tanzania Film Federation (TAFF), MFDI, Swahiliwood na makapuni ya usambazaji wa
filamu Steps Entertainment Ltd, Leo Media na kampuni mpya ya usambazaji ya
Proin Promotion ambayo imeanza hivi karibuni na kuonyesha dhamira ya kusaidia
tasnia ya filamu, pia leo tunazindua mtandao wa www.dff.or.tz
Kwa kutambua
mchango wako kama mwanahabari tunaamini utaungana nasi katika kuhakikisha DFF inakuwa ni chachu ya maendeleo ya
tasnia ya filamu Tanzania, huku tukisema kuwa Dar Filamu Festival2013 kwa kauli mbiuya ‘Ubora wa Filamu Zetu’ ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wote kwa
pamoja na kuwa jukwaa linalojenga tasnia ya filamu inayokua kila siku. Pia
tunaomba ushiriki wako katika kufanikisha hili.
Mratibu wa Tamasha la DFF 2013
Staford Kihore
Post a Comment