Video ya wimbo wa Iggy Azalea uliotengenezwa na Lovy Longomba ‘Change Your Life’


Mara ya kwanza nausikia wimbo mpya wa rapper raia wa Australia, Iggy Azalea, Change Your Life, niliupenda moja kwa moja. Ni ngoma yake ya pili niliyoipenda baada ya Work.
Nimekuja kufurahi zaidi baada ya kugundua kuwa producer na mwandishi wa wimbo huo ni mtu ninayemfahamu, Lovy Longomba, muimbaji wa kundi la Kenya, Longombas. Wow, kwakuwa nafahamu ugumu wa producer asiye na jina kutengeneza wimbo wa msanii wa mainstream nchini Marekani, mwili ulinisisimka na kutaka kufuatilia zaidi ni vipi amepata shavu hilo.
Niliamua kwenda mbali zaidi kutaka kujua mazingira ya yeye kupata nafasi hiyo na nikagundua kuwa, Lovy ni sehemu ama mwajiriwa wa Pulse Recordings yenye watunzi, waandishi na watayarishaji 37.
Feza
Kampuni hiyo huhusika na utunzi, uandishi na utengenezaji wa nyimbo. Kwahiyo wimbo wa Iggy Azalea umetengenezwa na Lovy kupitia mwamvuli wa Pulse Recordings. Lovy ameandika wimbo huo kwa kushirikiana na Raja Kumari wa kampuni hiyo pia. Cha kufurahisha zaidi ni kwamba, Lovy ni mwaafrika pekee kwenye kampuni hiyo na Change Your Life ni wimbo wa kwanza wa Lovy wa kimataifa. Hongera kwake.
Pulse Recordings kupitia waandishi wake imeshiriki kuandia hits kibao zikiwemo za Katy Perry, Demi Lovato, Ciara, Adam Lambert, Kelly Clarkson, Shakira, Carly Rae Jepse, Chris Brown, Beyonce, Pink, Alicia Keys, Madonna na wengi wengi sana.
Na sasa enjoy video ya wimbo huo hapo juu.

Post a Comment

أحدث أقدم