Baada ya show ya Kenya ‘kubuma’ Z-Anto aachwa kwenye mataa, alikosa hadi nauli ya kurudi Bongo

603385_275310915902008_1328507796_n
Kwa mujibu wa mtandao wa Niaje wa Kenya, muimbaji wa ‘Binti Kiziwi’ Z-Anto alipewa darasa la maana ya ‘Kuachwa Kwenye Mataa’ na promota wa Kenya aliyemchukua kufanya show kwenye miji ya Busia, Eldoret na Kitale pamoja na rapper wa Mombasa, Rapper Crazy K.
Show hizo hazikwenda kama zilivyokuwa zimepangwa baada ya muimbaji huyo kulalamika kuwa hakulipwa ujira wake kama walivyokubaliana.
Inadaiwa kuwa baada ya show ya kwanza iliyofanyika Alhamis iliyopita, Rapper Crazy K aliondoka na fedha zote na kumwacha Z-Anto akizunguka na kushangaa mataa ya mji wa Busia bila hata nauli ya bus kurejea Bongo.
Wilberforce wa Heart Beat Entertainment anadai ndiye aliyemsaidia muimbaji huyo kwa kumtumia fedha ya nauli ya kurudi nyumbani.
Hata hivyo, Crazy K amekanusha madai hayo na kusema kuwa Z-Anto ni muongo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook rapper huyo aliandika:
24th/2/2014(2:12pm) nlimtumia wilberfoce mwikya 24k, ampe z anto kutoka kwa evnt organiser. baada ya msanii kuchelewa nlimuuliza kwanini, z anto akanitumia ujumbe 3rd march at 3:54 pm akasema amepokea 20k pekee na hajui kwa nini, nlipomuuliza wilber akanijibu kwa txt kua si kweli. Ata ivyo z anto akasema atakuja kenya kufanya shw, japo hakuja wiki hiyo ata baada ya matangazo kuekwa. wakaelewana na promota kua iwapo pesa ya shws zilizobaki itarudisha hasara iliyotokea basi atapewa kitu kidogo, (not a must). Z anto alifanya shw moja pekee ambayo haikurudisha hata nusu ya garama iliyotokea na akasusia kufanya zengine. Gafla akaanza kupakaza kua mimi CRAZY K nimemtapeli. Naomba naye pia aende polisi aseme ni wapi tuliandikishana kua nafaa kumpa 20k zaidi, coz mimi nina txt zote za pesa nlizomtumia kupitia kwa wilberfoce mwikya

Post a Comment

Previous Post Next Post