Wanasayansi nchini Ufaransa
wamebaini kwamba virusi vya Ugonjwa wa Ebola ndio chanzo cha ugonjwa wa
homa ya haemorajic nchini Guinea ambayo inaaminika kuwauwa karibia watu
sitini.
Ugonjwa huo ambao unaweza kuambukizwa kwa haraka ulianza nchini humo yapata majuma sita yaliopita.Afisa mmoja wa wizara ya afya nchini Guinea amesema kuwa takriban visa vinane vya ugonjwa huo vimeripotiwa hususan kusini mwa taifa hilo.
Amsema kuwa serikali ya taifa hilo inatumia kila njia kukabiliana na ugonjwa huo lakini inaendelea kushindwa.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa Ebola ambao husambazwa kupitia kugusana na walioambukizwa.
Post a Comment