TIMU
za Barcelona na Real Madrid zote zimeongezewa nguvu kuelekea mchezo wa
leo usiku wa El Clasico kufuatia habari kwamba Gerard Pique na Karim
Benzema watakuwepo kwenye mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Santiago
Bernabeu, Madrid.
Beki
Pique hakuwepo wakati Barca inashinda 7-0 dhidi ya Osasuna kutokana na
maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia, lakini alirejea mazoezini Jumatatu
wiki hii.
Pamoja
na hayo, Carles Puyol, ambaye ataondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu,
atakosa mchezo ambao ungekuwa wa mwisho kwake dhidi ya Real kutokana na
maumivu ya goti.
Atakosekana: Carles Puyol anatarajiwa kuikosa 'El Clasico' yake ya mwisho akiwa na jezi ya Barcelona kutokana na maumivu ya goti
Neymar na Jordi Alba wakiwa mazoezini na wenzao wa Barcelona jana tayari kwa mchezo wa leo
Kiungo Alex Song akitaniana na Neymar kwa kumsukuma uwanjani huku Alba akitazama
Wote wanatabasamu: Gerard Pique alihudhuria uzinduzi wa albamu ya mpenzi wake, Shakira mjini Barcelona Ijumaa
Wakati
huo huo, mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema anatarajiwa
kurejea kwenye kikosi cha Los Blancos baada ya kukosa mechi timu yake
ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Schalke katika Ligi ya Mabingwa Jumanne.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Lyon alirejea kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancelotti
jana baada ya kuumia siku Madrid ikiilaza 1-0 Malaga ugenini.
Vinara
wa La Liga, Real wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wanawazidi kwa
pointi nne wapinzani wao hao, Barcelona walio katika nafasi ya tatu
nyuma ya Atletico wanaowazidi pia pointi tatu.
Wachezaji wa Real Madrid mazoezini jana
Nyota kweli: Lionel Messi akishuka Uwanja wa mazoezi wa Barcelona, Sports Centre jana kwenda kujifua kwa ajili ya mechi ya leo
Wataalamu: Kocha wa Barcelona, Martino (kushoto) na wa Madrid, Ancelotti nani ataipa ushindi timu yake leo?
Post a Comment