Mkurugenzi
Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akifafanua kwa waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utaratibu mpya wa wanafunzi
walionufaika na mikopo ya HELSB kurejesha mikopo yao kwa njia ya
mtandao kuanzia mwezi septemba 2013, ambapo huduma ya M-Mpesa ilianza
kutumika na kuanzia April 2014, Aitel Money itatumika pia kama mfumo wa
kurejesha mikopo hiyo. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo
Frank Mvungi.
………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imeanzisha utaratibu mpya wa kurejesha mikopo kwa njia ya mtandao.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wabodi
hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Mwaisobwa amesema kuanzia mwezi Septemba, 2013 Bodi hiyo ilianzisha
utaratibu mpya wa kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya M-Pesa.
Mwaisobwa
alisema katika kuimarisha mfumo wa urejeshaji mikopo kuanzia mwezi
april, 2014 walionufaika na mikopo hiyo wataweza kurejesha kupitia Aitel
Money.
Kabla
ya kuanza kutumia huduma ya M-pesa, mnufaika wa mkopo anapaswa
kuwasiliana na HELSB ili kupata mambo muhimu ambayo ni Taarifa ya Mkopo,
(Loan statement) Kiwango cha marejesho, (Loan instalments) na Namba ya
kumbukumbu (Loan number).
HELSB
pia hutoa msaada kwa waombaji wa mikopo wanaopata matatizo madogo
madogo wakati wa kujaza fomu kwa kutumia dawati maalum la msaada kwa
wateja ambapo msaada hutolewa kwa njia ya simu siku za Jumatatu hadi
Jjumaa kuanzia saambili asubuhi hadi saa 2 usiku.
Mwaisobwa
alibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili HELSB ni imani potofu
iliyoenea kwamba mikopo hiyo ni ruzuku na ushirikiano hafifu na baadhi
ya waajiri katika urejeshaji mikopo.
Mwaisobwa
alitoa wito kwa wale wote walionufaika na mikopo kurejesha mikopo hiyo
kwa wakati ili kutoa fursa kwa wahitaji wengine kukopeshwa.
Tangu
kuasisiwa kwake, Bodi hiyo imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya
wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla bodi kuanzishwa,
ambapo wanafunzi wameongezeka kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006
hadi wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013,ongezeko hili ni sawa na wastani
wa 10.4% kwa mwaka.
Post a Comment