.
Chama cha soka nchini Uingereza FA, kimemfungulia mashtaka meneja wa
klabu ya Chelsea Jose Mourinho, kwa madai ya tuhuma za utovu wa nidhamu
aliouonyesha wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza
uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Aston Villa ambao
walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Jose Mourinho anakabiliwa na mashtaka hayo baada ya kubainika aliingia uwanjani katika dakika ya tisini ya mchezo huo, ambapo imebainika alifanya hivyo kwa lengo la kupinga maamuzi ya muamuzi Chris Foy, ya kumuonyesha kadi nyekundu kiungo kutoka nchini Brazil, Ramires.
Taarifa iliyotolewa na FA, imeeleza kwamba meneja huyo, alifanya kitendo hicho kwa makusudi kutokanana kufahamu vyema kanuni na taratibu za soka ambazo hazimpi nafasi ya kutoka nje ya eneo lake la ufundi.
Hata hivyo chama cha soka nchini Uingereza FA, kimempa muda Jose Mourinho, hadi March 24 saa kumi na mbili jioni, kwa ajili ya kuyakubalia ama kuyakataa mashataka hayo, ili kupisha taratibu nyingine za kisheria kushukua mkondo wake.
Katika mchezo huo muamuzi Chris Foy, aliamuru Jose Mourinho kuondoka kwenye eneo la ufundi la klabu ya Chelsea, ikiwa ni sehemu ya adhabu ya kukiuka utatatibu kwa kuingia uwanjani.
Wakati huo huo, uongozi wa klabu ya Hull City unajiandaa kuwasilisha utetezi wa kupinga tuhuma zinazomkabili mshambuliji wao George Boyd ambae anatuhumiwa kwa kosa la kumtemea mate mlinda mlango wa klabu ya Man City Joe Hart, wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita.
Meneja wa klabu ya Hull City Steve Bruce, amesema watayapinga mashataka yanayomkabili Boyd, kwa nguvu zote kutokana na ushahidi walionao ambapo wanaamini utaweza kuwashawishi FA kufuta mashataka dhidi ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28
Post a Comment