Nyota Ndogo aongoza wanawake wa Kenya kwenye maandamano ya kupinga tabia ya Colonel Mustafa - Video

Mustafa
Muimbaji wa Kenya, Mwanaisha Abdallah Mohamed maarufu kama Nyota Ndogo, ameungana na wanawake wa Mombasa kufanya maandamano ya kupinga udhalilishaji dhidi yao unaofanywa na rapper, Colonel Mustafa ikiwa ni pamoja na kupost kwenye mitandao picha za wanawake wakiwa mtupu.
“Mimi naona kama Mustafa anatusi muziki, anatusi wanawake, anatusi mama yake. Kwahiyo Mustafa aombe msamaha kwa wanawake,” alisema Nyota Ndogo.
Mustafa anadaiwa kumtumia Huddah Monroe kujipatia umaarufu baada ya kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wana uhusiano wa kimapenzi. Baadaye Huddah alikanusha na kusema yote yalipangwa.

Post a Comment

أحدث أقدم