Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Jeshi la polisi
wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya
wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina
yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.
Mara baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako
maandamano yalikuwa yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla
polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa
jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo
alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali
wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini
nchini Paul Masanja kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.
Kufuatia malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali
gharama waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo
la machimbo ndipo mkutano ukavunjika na maandamano yakaanza na matokeo yake
mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto.
Katika na purukushani
hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa
risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na
mbunge huyo.
Katika hatua nyingine hali ilikuwa tete kwa waandishi wa
habari kwani askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari
kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia
baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.
|
Post a Comment