Mtu muhimu, bao muhimu; Mbwana Samatta ameifungia bao la ugenini Mazembe ikilala 2-1 Ivory Coast |
MSHAMBULIAJI Mbwana Ally Samatta usiku huu ameifungia bao muhimu timu yake, TP Mazembe ya DRC ikilala 2-1 mbele ya wenyeji, Sewe Sport ya Ivory Coast mjini Abidjan katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika. Wageni walitawala mchezo tangu mwanzo na mshambuliaji mwingine Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu alikaribia kufunga dakika ya tano kama, kama si jitihada za kipa wa Sewe, Sylvain Gbohouo kuokoa.
Ulimwengu aliyeanza leo katika safu ya ushambuliaji ya
Mazembe,
huku Samatta akianzia benchi, alisababisha misukosuko mingi langoni mwa
wenyeji, kwani dakika ya 17 aligongesha mwamba wa juu. Lakini
baada ya misukosuko hiyo, wenyeji walizinduka na kufanikiwa kupata bao
la kwanza dakika ya 38, mfungaji Roger Assale aliyeunganisha kwa kichwa
krosi ya Joseph Kadjo Kameni. Na Assale alikaribia kufunga tena dakika
mbili baadaye kama si kazi nzuri ya kipa wa Mazembe, Robert Kidiaba
kuokoa.
Thomas Ulimwengu aliitia misukosuko mingi lango la Sewe leo |
Sewekes
walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza bao 1-0 kabla ya kurudi kwa
hasira zaidi kipindi cha pili kusaka mabao zaidi kabla ya mchezo wa
marudiano mjini Lubumbashi wiki ijayo. Kocha
wa Sewe, Rigo Gervais aliwaingiza kiungo Hevra Kouassi na mshambuliaji
Hermann Kouao kuchukua nafasi za Ocansey Mandela na Zadi Wawa na hiyo
ikawasaidia kupata bao la pili dakika ya 82 lililofungwa na Christian
Kouame kwa penalti, baada ya Roger Assale kuangushwa kwenye eneo la
hatari na Jean Kasusula. Lakini
The Corbeaux walifanikiwa kupata bao la ugenini dakika mbili kabla ya
filimbi ya mwisho kupitia kwa Samatta aliyetokea benchi na sasa Mazembe
watahitaji ushindi wa 1-0 tu nyumbani Lubumbashi katika mchezo wa
marudiano wikiendi ijayo ili kutinga Hatua ya Makundi.
Post a Comment