TANGAZO LA TELECONFERENCE KWA WATANZANIA WOTE WAISHIO MAREKANI


Waheshimiwa Wanadiaspora,
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania za Marekani wakishirikiana, ZADIA na DICOTA, wanapenda kuwatangazia kuwa kutakuwa na teleconference siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi kuanzia saa mbili usiku(8:00PM) kwa saa za Eastern Time.
Lengo ni kuwapa muhtasari wa masuala yanayoendelea kule Dodoma kwenye Bunge Maalum la Katiba na kuwafahamisha mpaka sasa tumefikia wapi katika kuhakikisha suala la uraia pacha linaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watanzania na Watu wenye asili ya Kitanzania wanaoishi Marekani wote mnaombwa kuudhuria.
Ili uweze kushiriki kwenye Teleconference hii piga namba 712-432-1500 halafu ingiza pin namba ikifuatiwa na alama ya reli kama ifuatavyo: 465228#.
Wote mnakaribishwa.
Imetolewa na:
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Marekani, ZADIA na DICOTA.
Tarehe 18 Machi 2014.

Post a Comment

Previous Post Next Post