Na Georgina Misama-MAELEZO
Serikali imesema inatambua Tasnia
ya Filamu ikiendelezwa vizuri ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na
ni njia madhubuti ya kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa kitenngo cha mawasilianao serikalini
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Concilia Niyibitanga
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyikia ukumbi wa Idara ya
habari MAELEZO.
Concilia alisema kuwa mwamko unaongezeka kwa wasanii na watengenezaji wa filamu kutoka ndani na nje ya nchi.
Hii inajidhihirisha kwa idadi ya vibali vya utengenezaji filamu imeongezeka kutoka 100 mwaka 2000 hadi 472 Januari 2014.
Aidha,
kampuni zinazojishughulisha na uendeshaji wa shughuli za filamu nchini
zimeongezeka kutoka Kampuni moja ya Filamu Tanzania (TFC) na kufikia 129
mwaka 2013.
Kwa
upande wa watengenezaji wa filamu za ndani, uwasilishaji wa ukaguzi
umeongezeka kutoka filamu 96 mwaka 2000 hadi kufikia 1059 Februari 2014.
Naye
Katibu Mtendaji wa Bodi ya filamu nchini Joyce Fisoo alitoa rai kwa
wasanii wa filamu kutumia lugha ya Kiswahili hasa katika uandaaji wa
jina ili kulinda na kuikuza lugha yetu ya Kiswahi.
Tasnia
ya Filamu nchini ilianza tangu mwaka 1920 wakati wa ukoloni, baada ya
Uhuru, Serikali ya Tanzania kupitia bunge iliamua kutunga sheria namba 4
ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya kuigiza ili kuweka usimamizi
mzuri wa tasnia hiyo.
Post a Comment