Tigo yatoa msaada wa vitabu vya 6m/- kwa shule ya msingi Kilimani – Dar


1 (8)
Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael akiwakabidhi msaada wa vitabu, Happiness Mathias (kushoto) na Ibrahim Issa, wanafunzi wa shule ya Kilimani, iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam mapema jana. Akishuhudia katikati yao ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zubeda Jeni. Tigo ilikabidhi msaada wa vitabu 905 vyenye thamani ya milioni 6.1 na tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 kwa shule hiyo.
2 (3)
Mratibu wa Elimu wa kata ya Manzese Bi. Petronila Liyamuya (kulia) akipitia moja ya vitabu vilivyokabidhiwa na Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael (kushoto) katika shule ya msingi Kilimani, Manzese. Katikati ni  Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani Bi. Zubeda Jeni. 
Katika jitahada za kusaidia kuboresha hali ya maisha ya watanzania kupitia kuwekeza katika mipango ya maendeleo ya kijamii, Tigo Tanzania leo imetoa msaada wa vitabu vya wanafunzi wa darasa la nne hadi la saba vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1/- kwa shule ya msingi Kilimani iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo katika shule hiyo, Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Tigo, Woinde Shisael, alisema kwamba kampuni hiyo ya simu inatambua fika umuhimu wa elimu kama kiungo muhimu katika kuchangia mabadiliko kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
Woinde pia alikabidhi, tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 4,000 za maji la thamani ya shilingi 653,000/-, pesa iliyokusanywa kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Alisema msaada huo utachangia kuboresha mazingira bora yakujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu shuleni hapo.   
3a (1)
Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese Bi. Zubeda Jeni (kushoto) akimshukuru Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael kwa msaada wa tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 yenye thamani ya Tsh 653,000/- pesa iliyochangishwa na wafanyakazi wa Tigo. 
“Kama inavyoeleweka kwamba elimu ni ufunguo wa maisha ya mtu, jamii na hata taifa zima kwa ujumla, ndio sababu Tigo inapenda kutoa msaada huu kwa wanafunzi wa shule hii ili kuwawezesha kutimiza ndoto hii,” alisema Shisael.
Ukiondoa sekta ya elimu, Tigo pia inasaidia sekta zingine za kijamii zikiwemo afya, kutengeneza ajira na ujasiriliamali jamii, mipango ambayo kwa mujibu wa Shisael imeweza kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania nchi nzima.
Akipokea msaada huo, mwalimu mkuu wa shule hiyo Zubeda Jeni, aliishukuru Tigo kwa msaada huo akisema kwamba msaada wa vitabu hivyo utasaidia kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa msaada huu ambao tunaamini utasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi na walimu katika kutimiza malengo yao ya kufaulu vizuri katika mitihani yao,” alisema Jeni. 
4a
 Risala ikisomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kilimani Bi. Zubeda Jeni ambapo aliishukuru kampuni ya simu Tigo kwa msaada wa vitabu na tenki la maji iliyotolewa. Mwalimu mkuu huyo alisema msaada huo uliotolewa ni kitendo cha kizalendo kilichofanywa na anaamini kwamba vitabu hivyo vitaongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi walio darasa la nne na la saba wataonufaika moja kwa moja na msaada huo.  
5a
Wafanyakazi wa Tigo katika picha ya ukumbusho na wanafunzi na walimu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Tigo ilifika mapema jana kutoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1 pamoja na tenki la kuhifadhia maji yenye uwezo wa kubeba lita 4000.
6a
Wanafunzi wa darasa la nne na la saba wa shule ya msingi Kilimani wakiimba wimbo wa “Tanzania, Tanzania” kama ishara ya uzalendo na kutambua mchango wa Tigo kama kitendo cha kiungwana kwa shule hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post