UKWELI KUHUSU KITUO KIPYA CHA REDIO, 93.7 FM DAR ES SALAAM

Fundi wa Ujerumani akijaribu mitambo kwenye studio za kituo hicho cha redio kilichopo Kawe, Dar
Katika kile kinachoonekana ujio wa redio mpya jijini Dar es Salaam, uvumi umeanza kusambaa juu ya kituo hicho kipya cha habari ambacho jina lake bado halijafahamika rasmi.
Kwa mujibu wa viashiria habari mbalimbali na minong’ono inayoendelea jijini Dar es Salaam, masafa ya redio 93.7 FM DSM yamekuwa gumzo katika viunga mbalimbali ambapo watu wengi wameingiwa shauku ya kutaka kujua redio hiyo inaitwaje na watangazaji wake ni akina nani!
Pamoja na kutojua kwa undani maudhui kamili ambayo redio hiyo itatumia katika vipindi vyake, kwa mujibu wa utafiti wa haraka haraka na wa chini chini tuliojaribu kuufanya dalili zinaonyesha kuna mtazamo wa kiburudani zaidi kwa namna moja ama nyingine, kwa kuwa, baadhi ya maswali ambayo ndiyo msingi wa minong’ono ambayo watu wengi wameyasoma kupitia akaunti ya twitter ya masafa hayo @New937.

Baadhi ya maswali hayo yamekuwa yakiwataka wananchi kuchagua playlist za nyimbo wanazozitaka ama kuzipenda na pia maswali yanayohusu aina ya watangazaji ambayo wananchi wanapendelea na upepo kuegemea zaidi kwa wasanii wa Bongo Flava Bongo Movie.
Inaeleweka mara nyingi kuwa redio mpya mara nyingi huvutia baadhi ya watangazaji, ma Dj, maprodyuza na hapo ndipo swali la je kuna uwezekano wa watangazaji na ma Dj nguli ambao tunaweza kuwasikia wakiibukia katika redio hiyo?
Tayari masafa hayo ya 93.7 FM DSM yameshaanza kuteka hisia za wakazi wa jiji la Dar baada ya picha na video kadhaa za studio ambapo matangazo ya redio hiyo yatakuwa yakirushwa kuonekana kupitia mtandao wa twitter na pia kwa wahusika kuthibitisha uwekaji wa nyimbo laki moja katika database ya redio hiyo.
Moja ya wadau wa burudani na sanaa ambaye tuna hisi anaweza kuwa na uhusiano wa karibu kabisa na umiliki ni Lady Jaydee ambaye minong’ono inamzungumzia.

Post a Comment

Previous Post Next Post