Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amezindua kampeni ya
uchaguzi wa Urais kwenye jiji la Barranquilla, lakini wakati akihutubia,
janga likamtokea.
Rais huyo alikuwa akihutubia kwa mzuka kabla ya kujikojolea hadharani
na kila mtu akiona japo hakusitisha hotuba hiyo. Video yake imekuwa
maarufu tayari mtandaoni. Hata hivyo Rais huyo amekanusha kuwa na
matatizo ya kiafya. Ametumia mtandao wa Twitter kuwashakuru wananchi wa
Colombia kwa kumuelewa licha ya aibu hiyo.
Rais huyo mwenye miaka 62 aliwahi kufanyiwa upasuaji kutokana na saratani korodani (prostate cancer).
Post a Comment