Waimbaji walioacha muziki tunaopenda warudi tena – Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyinn

gEs60KRbMaisha, majukumu, uzazi na mambo mengine, yamewafanya wasanii wengine kuacha muziki na kuendelea na shughuli zingine zikiwemo za ujasirialimali ama za ofisini. Wengine wameacha baada ya kuona pamoja na kufanya muziki mzuri, kile kinachopatikana hakiwezi kufuta jasho la jitihada zao na kwakuwa maisha lazima yaendelee. Bahati mbaya ama nzuri, baadhi ya wasanii waliacha muziki wakiwa bado kwenye peak na hivyo kufanya kuwa na ‘demand’ kubwa ya nyimbo zao mpya kwa mashabiki wao.
Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyinn
Wakati K-Lyinn anafanya muziki, hakuna ubishi ndiye alikuwa mwanamuziki mrembo zaidi nchini Tanzania. Pengine ilikuwa ni surprise kwa wengi nikiwemo mimi niliyekuwa namfahamu zaidi kwa nafasi ya Miss Tanzania (2000) kubaini kuwa kumbe ni mwanamuziki mzuri pia.
Lakini kile ambacho nilikuwa sifahamu ni kwamba K-Lyinn alianza kuimba hata kabla ya kushinda taji hilo.
Alianza muziki kwa kuimba na bendi ya Tanzanites ambako alikuwa muimbaji mkuu kwa miaka mitatu. Akiwa na bendi hiyo aliwahi kufanya ziara katika sehemu mbalimbali duniani zikiwemo Dubai, Bahrain na Abu Dhabi.
Mwaka 2004 aliachia album yake ya kwanza ikiwa na hit kama “Nalia Kwa Furaha” aliyomshrikisha Bushoke. Wimbo huo ulifanya vizuri mno na hadi sasa video yake inabaki kuwa miongoni mwa video za muziki za wasanii wa Tanzania zilizoangaliwa sana kwenye Youtube ikiwa na views zaidi ya 1,303,080. Pia kwa miaka 7 iliyopita, hakuna ubishi ilikuwa ni video bora kabisa kwa Tanzania na pengine urembo wake ulifanya video ivute attention ya watu wengi.
Nalia Kwa Furaha haikumfanya K-Lyinn kuwa ‘one hit wonder’ kwakuwa baada ya miaka mitatu alikuja kutawala tena mawimbi ya redio kwa wimbo wake ‘Crazy Over You’ aliomshirikisha Squeezer. Video yake pia ilitengeneza muelekeo mwingine wa video bora za muziki za Tanzania na tena urembo wake kwenye video hii ulivutia wengi.
Hakuishia hapo tena, K-Lyinn aliendelea kuachia hits nyingine kibao ukiwemo ‘Chochote Utapata’ aliomshirikisha rapper wa Chamber Squad, Noorah aka Babastylez.
“Kwa mimi ninavyomuona ni mtu aliyekuwa anajua nini anachotaka kufanya,” anasema Noorah.
“Wimbo ulipokelewa vizuri sana yaani, tofauti na nilivyokuwa natarajia, sikudhani kama ungekuwa mkubwa.”
Noorah anasema hadi sasa K-Lynn ana mashabiki wengi wanaomhitaji arudi tena. “Mashabiki ni watu ambao wana nguvu yao kubwa sana. Unaweza ukawa umefanya nini, sijui umefikia wapi kwenye maisha yako lakini mashabiki kama wamekupenda, wamekupenda tu na mimi kimtazamo wangu naona walimpenda sana, kwa mapenzi waliyokuwa nayo juu yake, obvious bado wanamuhitaji.”
Mr Blue ni msanii mwingine aliyeshirikishwa na K-Lyinn kwenye wimbo wake ‘Nipe Mkono’ ambao nao ulifanya vizuri.
“Mara ya kwanza nilimuona akiwa anahojiwa na nikamsikia akisema ‘bana katika watu ninaopenda kufanya nao kazi ni Mr Blue, tukifanya kazi pamoja itakuwa ni vizuri,” anasema Blue.
“Mwisho wa siku akanipigia simu na tukaonana ndio tukaifanya hiyo kazi pamoja. K-Lyinn ni mtu anayejituma, anafuatilia kazi yake kwa makini na nini, mimi nashauri ni vizuri akirudi. Kama alifanya kwaajili ya mashabiki basi asiwaache njia panda. Siwezi kusema anafanya kwaajili ya pesa atakuwa hana shida, lakini kama atafanya kwaajili ya mashabiki aendelee tu.”
Ni kweli K-Lyinn hana shida kwakuwa kwa sasa ni mchumba wa miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa Forbes, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi ambaye wamejaaliwa watoto mapacha wa kiume. Pamoja na hivyo, Jacky ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni yake ya mapambo ya ndani, Amorette Ltd.
Kuna uwezekano akarejea tena kwenye muziki? Sio rahisi. Baada ya kuulizwa sana swali la kwanini aliacha muziki, June mwaka jana, K-Lyinn aliitaja sababu.
“Huwa naulizwa sababu ya kuacha muziki,mojawapo ilikua ni ukandamizwaji na kutopewa haki kama msanii.Natumaini waliobaki watapigania haki,” alitweet K-Lyinn.
Kwakuwa Miss Tanzania huyo wa zamani aliacha muziki akiwa kwenye peak, bado anachukuliwa kama miongoni mwa wasanii bora wa kike kuwahi kutokea nchini na ana mashabiki wengi.
Kazi zake zingine..
Besti
Nikipata Wangu

Post a Comment

Previous Post Next Post