Warusi zaidi wawekewa vikwazo na EU

Marekani yaongeza vikwazo kwa Warusi
Viongozi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Ulaya wanaokutana mjini Brussels kuimarisha vikwazo
wanavyowekea Urusi,wameamua kuongeza idadi ya Warusi wanaopaswa kuwekewa vikwazo kibinafsi.
Orodha ya awali ya 21 sasa imeongezewa watu wengine 12.
Viongozi hao wa Jumuiya ya Ulaya pia wametoa wito kwa Tume inayosimamia jumuiya hiyo iwe tayari kuimarisha vikwazo
zaidi vya kiuchumi dhidi ya Urusi iwapo hali hiyo ya sintofahamu itaendelea.
Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema kuwa wale ambao majina yao yameongezwa kwa orodha ya hapo awali
hawataruhusiwa kutembelea Ulaya na mali yao itapigwa tanji kama ilivyofanyika kwa maafisa 21 wa Urusi na Ukraine
mapema juma hili.
Bi Merkel pia alisema kuwa Jumuiya ya Ulaya iko tayari kuunga mkono Serikali mpya ya Ukraine kifedha, bora tu iafikiane
na Hazina ya Fedha duniani (IMF). Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema hatua muhimu zimechukuliwa
kufikia sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post