Miongoni
mwa sababu nyingi zilizonifanya kutangaza uamuzi huo ni sintofahamu
iliyozuka ndani ya klabu yetu, kwa taaluma yangu ya uandishi wa habari
lazima niwe na msimamo juu ya mambo yanayoendelea kwenye jamii.
Ili
niendelee kufanya kazi na klabu hii kwa wakati huu wa misuguano, lazima
niwe na upande; kwa maana upande unaounga mkono uongozi ama upande
usiokuwa na Imani na uongozi. Lakini mimi nimeamua kutounga mkono upande
wowote.
Kwa hivyo basi, ili niwe katika mstari sahihi nimeamua kukaa pembeni nifanye shughuli zangu za uanahabari kwa furaha na amani.
Bado
ni mwanachama halali wa Coastal Union Sports Club, namba yangu ya kadi
ni 0013. Nitaendelea kutoa ushauri na kuishabikia klabu yangu ambayo
nimekuwa nikimuona marehemu baba yangu na kaka zangu wakiishabikia tangu
nikiwa mdogo.
Mtashangaa
nimetangaza uamuzi huu wa kuachia ngazi bila kusema kuwa nimeandika
barua ama la, kifupi sina mkataba wala taarifa yoyote ya kimaandishi juu
ya kuajiriwa kwangu na klabu. Hivyo nimeamua kujiuzulu kienyeji kama
nilivyoitwa kienyeji.
Post a Comment