Siku zote katika maisha yangu tokea nimeanza kazi ya muziki, nimekua na shauku kubwa sana kutaka FANS wangu muweze kunijua na kujua kila kitu ninachokifanya katika maisha yangu hata ikiwezekana kila siku iendayo kwa mungu kuweza kuona Mrap Lion anafanya nini, lakini nafasi ni ndogo sana ila ntatumia nafasi hii kuweza kukuweka karibu wewe shabiki yangu sababu najua hamu yako kutaka kujua MRAP anafanya nini.
Naitwa “Richard Alibalio Prudence” also known as, Mrap Lion, mzaliwa wa jijini Dar Es Salaam katika hospitali ya Muhimbili. Nimepata elimu yangu katika mikoa tofauti nchini Tanzania ikiwemo Kagera, Zanzibar na Dar katika shule za Rubya Seminary – Kagera, Francis Maria Secondary School – Zanzibar na Jitegemee High School – Dar, nilipomalizia elimu yangu ya sekondari na sasa nipo chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) mwaka wa kwanza nikichukua “Bachelor Degree of Insurance and Risk Management”
Nimeanza kufanya kazi zangu za muziki mwaka 2010 kipindi nipo elimu ya sekondari na kufanya kazi na studio za mtaani na kufikia kufanya kazi na studio kubwa zikiwemo AM Records chini ya Producer Manecky na Bob Manecky, BHitz studio inayomilikiwa na Producer Hermy B chini ya Producer Pancho Latino ambae aliniona kwenye nyimbo niliyofanya na Makamua chini ya Producer Manecky ijulikanayo kama “Tunamaintain”. Baada ya kufanya kazi na studio hizo hivi sasa nafanya kazi zangu mwenyewe chini ya usimamizi wa aina tofauti kabisa na kazi nyingi za aina tofauti zimeshafanyika na tunaendela kufanya zaidi kwa ajili ya nyie Fans wangu ambao naamini kabisa kila ninachofanya ni kwa ajili yenu.
“MRAP LION” ni jina lililotokana na majina yangu mwenyewe binafsi niliyopewa na wazazi wangu ambapo ‘M’ inatokana na “Mwijage”, ‘R’ Richard, ‘A’ Albalio, ‘P’ Prudence na LION imetokana na NYOTA yangu “LEO” (SIMBA) sababu nimezaliwa tarehe 18 mwezi wa 8 (August).
Kama msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya ujulikanao kama “Hip Hop”, kuna vitu vingi sana na mipango endelevu kimuziki huku nikiendelea na masomo yangu. Mwaka huu wa 2014 kuna mipango mingi sana kwa kudokeza tu kuwa nje ya usanii wa muziki vile vile nimeanza kufanya kazi kama ‘Actor’ ambapo nimeshafanya ‘Short Film’ ambayo ni kwa ajili ya mafunzo kwa jamii katika mlengo wa utumiaji wa madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya kwa sasa yanahatarisha maisha ya vijana wengi hapa nchini na ambao ndio Taifa la kesho la Tanzania. Filamu hii imenuia na madumuni yake ni kulenga wanafunzi wa Nyanja tofauti ambao ndio wenye nguvu na tegemeo la taifa la kesho la nchi yetu, uzinduzi wake pamoja na mipango iliyopangwa katika shunguli hii itawalenga wanafunzi kuanzia ngazi ya Sekondari. Mengine zaidi ya kazi hizi yatawajia zaidi wakati muafaka.
Mwisho kabisa napenda sana kushukuru mashabiki wangu (Fans) sababu kama nilivyosema mwanzoni bila nyinyi siwezi kuwa Mrap LION anaeandika barua hii kwenu, nipo kwa ajili yenu na hakuna siku ambayo nitakuwa mimi bila nyinyi, nashukuru sana sana kwa support mnayonipa tokea nimeanza mpaka hivi sasa, sister fetty, So So FRESH na CLOUDS MEDIA GROUP, Madj, bloggers na wengine wote katika Media na Entertainment mnaofanya kazi ya kusaidia muziki wangu kuwafikia Fans wangu popote pale walipo. ASANTENI SANA.
GOD Bless You ALL
Post a Comment