Mtanzania Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa
kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki
wenzake watatu wa kike wakitoka mchezoni.
Sabina, Lilian, Esther
Esther (Uganda) , Lilian (Nigeria) pamoja na Sabina (Kenya) ndio
washiriki walioondolewa katika shindano hilo usiku wa jana ikiwa ni
‘eviction’ ya pili toka shindano lianze.
Hadi sasa washiriki watano wa kike wametoka katika shindano hilo na
kufanya idadi ya washiriki wa jinsia ya kike kubaki 8 huku wanaume
wakiwa 13.
Nchi za Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda and Nigeria kila moja
imeshapoteza muwakilishi mmoja hivyo zote zimebaki na muwakilishi mmoja
mmoja tu mjengoni.
Post a Comment