Serikali
ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa
Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Mkuu wa
jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa
mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa
wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana
na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur
ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na
wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais
wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram wamekubali
kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo,
maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine
utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba
maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba
wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa
Boko Haram, Abubakar Shekau.
Post a Comment