HARUSI YA KWENYE HELIKOPTA YAACHA GUMZO ROMBO KILIMANJARO

Maharusi wilayani hapa wameacha gumzo baada ya kukodi helikopta kutoka Kenya kunogesha harusi yao na kuruka angani.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri katika mji mdogo wa Tarakea uliopo mpaka wa Tanzania na Kenya. 

Maharusi hao, Lameck Yesse na Gladmarry Mushi walivuta hisia za wengi kwa kuwa bwana harusi ni dereva wa gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah analolimiki na bibi harusi ni mwanafunzi wa chuo jijini Arusha.
Mashuhuda walisema tukio hilo ni la kwanza na la aina yake katika mji huo. 

Maharusi hao walifunga ndoa katika Usharika wa Tarakea wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), na ibada iliongozwa na Mchungaji Emmanuel Dediok.

Post a Comment

Previous Post Next Post