Tanzania inatarajia kuanza kuona makampuni ya simu yakiweka hisa
zake kwenye soko la hisa kupitia sheria ya lazima inayolenga kuwasaidia
wananchi wake kumiliki sehemu ya moja viwanda vinavyokua kwa kasi zaidi
barani Afrika.
Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, January Makamba
yupo kwenye hatua za mwisho ya kuhakikisha makampuni ya simu yanaweka
hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, DSE.
Makamba ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kuwa hatua hiyo itaanza mwakani.
Sheria inayataka makampuni ya simu kuwa yameweka hisa zake hadi
kufikia mwaka 2013 lakini utekelezaji wa hatua hiyo uliahirishwa
kutokana na masuala ya kisheria.
Mkurugenzi Mkuu wa DSE, Moremi Marwa, amesema mpango huo wa makampuni kuweka na hisa zake sokoni utakuwa na faida kubwa.
Post a Comment