Mechi ya Ligi Kuu ya
Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga
na Simba iliyochezwa juzi
(Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh.
427,271,000.
Washabiki 49,542 walikata
tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio
vilikuwa sh. 7,000, sh.
10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya
Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati
asilimia 5 ya gharama ya
tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.
Kwa upande wa Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh.
1,000 kwa kila tiketi,
timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho
la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo mwingine wa mapato
hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za
mchezo sh. 24,751,024.01,
Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh.
17,471,311.07, DRFA sh.
10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh.
100,460,038.64 na timu
ngeni Simba sh. 71,341,186.86.
*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA*
Post a Comment