Katika hali isiyokuwa ya kawaida,
mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi wilayani mbeya
amenunua mbuzi wawili na bidhaa nyingine za aina mbalimbali zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na kuzipeleka kwenye vituo vya
watoto yatima kama zawadi huku akiwaasa watoto hao kutoshawishika
kwenda kupiga debe kwenye vituo vya mabasi.
Mpigadebe
maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi, Anganile Mwamuluma Andrea
ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ameushangaza umma wa
wakazi wa mbeya baada ya kuamua kununua mbuzi wawili, mchele, maharagwe,
sabuni, mafuta ya kupikia na mahindi na kupeleka bidhaa hizo katika
vituo viwili vya watoto yatima ambako amezitoa kama zawadi kwa watoto
hao, huku akiwaasa kutoshawishika kujihusisha na kazi ya kupiga Debe
kwenye vituo vya mabasi.
Walimu wa watoto hao wameeleza kushtushwa na kitendo cha mpigadebe huyo, lakini wakasema kuwa ni mfano Bora wa
kuigwa kwa vijana wanaofanikiwa kukumbuka mazingira walikotoka, huku
wakiwahimiza wazazi kuongeza upendo kwa watoto wao ili kupunguza wimbi
la watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini.
Baadhi
ya watoto ambao wamepokea msaada huo, wamemshukuru mpigadebe huyo na
kuwataka watu wengine kupata funzo la kuthamini na kuwapenda watoto
ikiwa ni pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri ya kujitegemea.
Post a Comment