Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo
Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete leo ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Kitanzania
23 miongoni mwa maafisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo
liliwajumuisha maafisa wa kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka
Kongo.
Jumla
ya wanajeshi 414 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamehitimu
mafunzo ya Uafisa katika chuo cha maafisa (TMA) Monduli baada ya
kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja.
Maafisa
hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa
watanzania 23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu
baada ya kula kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Tofauti na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 23 .
Aidha,
leo hii kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi
kutunukiwa kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa wa kongo
wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na wakiwa katika ardhi yao, hivyo
wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.
Akitoa
shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye
alishuhudia maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru
kwa kukubali kutoa mafunzo kwa maafisa hao.
Pia
alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia
kuimarisha usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha
amani nchini Kongo.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe.
Dkt Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri
Mkuu Mstaafu na mbunge waMonduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Bw. Magesa Mlongo, majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi
wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
kwa
upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri
wa Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond
Tshibanda N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma
Alfani, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa
Mafunzo, ya Kijeshi, brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.
Post a Comment