Rais Kikwete azindua kijiji cha mfano cha vijana Sikonge mkoani Tabora


unnamed (1)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge jana.Rais Kikwete yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za Mwenge leo.watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selenga.
unnamed (2)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana wajasiriamali katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora.
unnamed (3)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.
unnamed (4)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano.
unnamed (5)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano. (Picha na Freddy Maro).

Post a Comment

Previous Post Next Post