Amiri Jeshi Mkuu,
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi
wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi
kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014
Maafisa wapya wa
jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni
kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika
chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha
Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi ofisa kadeti Yusup
kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati
wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli jana.
Rais Joseph Kabila
wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada ya kuibuka
mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya kutunuku
kmaisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika
Chuo cha kijeshi monduli leo.
Amiri Jeshi Mkuu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya
kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC
yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange wakisimama kikakamavu wakati nyimbo za taifa
za nchi hizo zikipigwa wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku
kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha
kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Picha na Fred Maro
Post a Comment