Kampuni ya Samsung ya Korea Kusini imetengeneza teknolojia ya 60
GHz ya WiFi ambayo itaweza kutuma data mara tano zaidi ya vifaa
vingine.
Kifaa hicho kitakuruhusu kutuma data zenye ukubwa wa megabytes (MB)
575 kwa sekunde 1 – ambapo ni sawa na kudownload filamu ya GB 1 kwa
sekunde 3 tu.
Hiyo inamaanisha kuwa video zenye ukubwa na za high-definition
zinaweza kuangaliwa kutoka kwenye simu kwenda kwenye TV katika muda huo
huo real-time.
Teknolojia ya Wi-Fi iliyopo sasa ni ya 2.4 GHz na 5 GHz
Post a Comment