Na Faustine Ruta, Bukoba
Jumla ya wachezaji 26 wa Timu ya Stand
United waliotua Mjini Bukoba Jana kwa ajili ya Kipute cha Ligi kuu
Vodacom msimu wa 2014-15 na Wenyeji wao Kagera Sugar wamefanya mazoezi
yao kwa mara ya kwanza Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba.Wachezaji
hao 26 wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na Viongozi
wengine 6. Timu ya Stand United ya Shinyanga ni miongoni mwa timu tatu
zilizopanda Ligi na kesho Jumamosi inataka Kuibana Timu ya Kagera Sugar
ambao ndio wenyeji wao ambao pia wanashikilia nafasi ya sita kwenye Ligi
hiyo ya Vodacom kwa msimu huu ulioanza hivi karibuni. Hii itakuwa Mechi
ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Kagera wanaingia wakiwa nafasi ya
nne na pointi zao 4 huku Stand United wakiwa nafasi ya 8 nao wakiwa
wanalingana pointi na Kagaera Sugar.Wachezaji
wa Stand United wakifanya mazoezi yao ya Mwisho kwenye Uwanja wa
Kaitaba Bukoba Mjini tayari kwa kuumana na Wenyeji wao Kagera Sugar
kesho Jumamosi tarehe 18, 2014.Stand UnitedWachezaji wa Stand United
wakifanya mazoezi Stand United wakipasha tayari kwa kipute na Kagera SugarVijana wa Timu ya Stand United ya Mjini Shinyanga wakijifua kwenye Uwanja wa Kaitaba leo Ijumaa tayari kwa mtanange wao na
Kagera hapo Kesho jumamosi.Kocha
Mkuu wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe (kushoto) akiwacheki
Vijana wake Wakijifua kwenye Uwanja wa Kaitaba leo Ijumaa Jioni. Kocha Mkuu wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe akisimamia kazi yake ya Ukocha kwenye Uwanja wa Kaitaba leo. Kesho tunataka Ushindi tuu!!Kocha akiteta na Wachezaji wake
STAND UNITED WATUA BUKOBA! WAFANYA MAZOEZI KAITABA TAYARI KWA KUUMANA NA KAGERA SUGAR KESHO JUMAMOSI
Hisia
0
Post a Comment