MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA TUNSUME MBOPE
(35) MKAZI WA KYELA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.496 CRL AINA YA KINGLION ILIYOKUWA
IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
16.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO MAFULA SOP, KATA YA KYELA,
TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA KYELA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
YA WILAYA YA KYELA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 05
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ISACK JACOB MKAZI WA KIJIJI CHA ILUNDO
ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA MTI ULIOKUWA UNAKATWA NA
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KIWIRA ILIYOPO WILAYA YA RUNGWE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
16.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO YA SHULE YA
SEKONDARI KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIKUWA
AKIOKOTA KUNI NA WATOTO WENZAKE VICHAKANI NA NDIPO ALIANGUKIWA NA MTI
HUO NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA
MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUTOWARUHUSU
WATOTO WADOGO KWENDA MAENEO YA VICHAKANI/PORINI BILA KUWA NA WATU WAZIMA
KWANI NI HATARI.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, WATU WANNE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ZAKAYO NOVA (27) 2. HAMADI NGEKA (27)
WOTE WAKAZI WA TUNDUMA 3. YONA SIWALE (23) MKAZI WA KIJIJI CHA CHIWANDA
NA 4. EZEKIA SIKAPONDA (33) MKAZI WA CHITETE WANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NG’OMBE WANNE WANAODHANIWA KUWA MALI YA
WIZI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI HUKO KATIKA MACHINJIO YA
TUNDUMA, MTAA WA SOGEA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA
WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, NG’OMBE HUO NI MALI
YA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUSANGIA JIHUMBI, MKAZI WA
CHITETE. AIDHA, THAMANI YA HALISI YA NG’OMBE HAO NI TSHS.2,400,000/=.
NG’OMBE HAO WAMEHIFADHIWA KITUO CHA POLISI TUNDUMA WAKISUBIRI TARATIBU
NYINGINE ZA KISHERIA.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA RAIA WA NCHINI MALAWI
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI
KINYUME CHA SHERIA. MHAMIAJI HUYO AMEFAHAMIKA KWA JINA LA ALFRED RUNGU
(40) ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA 08:50 ASUBUHI HUKO
STENDI YA MABASI TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU
MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA
UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA RIFT VALLEY WILAYA YA
CHUNYA AITWAYE LUCY EDWARD (25) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 20.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
16.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA RIFT
VALLEY, KIJIJI CHA MALANGAMILO, KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA
YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI NA MUUZAJI WA POMBE
HIYO.
KATIKA MSAKO WA NNE, MTU MMOJA MKAZI WA CHIANGA NCHINI ZAMBIA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEORGE SIKAMANGA (18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 85 NA GRAMU 10 ZA BHANGI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
16.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:45 JIONI HUKO ENEO LA CUSTOM, KATA NA TARAFA
YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA
JESHI LA POLISI KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI HIYO
NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI/DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment