SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema
hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati yake na mamlaka husika nchini
Tanzania za kuwezeshwa kujengwa kwa bwawa la kufua umeme la Stiegler’s
Gorge .
Ofisi
za Shirika hilo zilizopo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki wametoa
taarifa ya kukanusha maelezo yaliyoandikwa na gazeti la The Guardian
(ref:http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=72984) kwamba yapo maafikiano kuhusu ujenzi wa bwawa hilo.
Eneo
la Stiegler’s Gorge lipo katika hifadhi ya Selou ambayo ni sehemu ya
urithi wa kimataifa ambapo ujenzi wa miundombinu yoyote yenye athari
kubwa katika hifadhi hiyo lazima kuwepo na maridhiano kati yake na
mamlaka husika.
Taarifa
hiyo imesema taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo Oktoba 8, mwaka huu
limeshutua shirika hilo. Taarifa hizo zilizokuwa ukurasa wa mbele
zilisema kwamba Tanzania itavuna zaidi nishati ya umeme kutokana na
maafikiano yake na UNESCO juu ya ujenzi wa wa bwawa hilo.
Katika
taarifa yake UNESCO imesema kwamba katika mkutano wa 36 wa kamati ya
Urithi wa dunia (WHC) uliofanyika Saint-Petersburg mwaka 2012 na ule wa
37 uliofanyika Phnom Penh, mwaka 2013 na wa mwisho uliofanyika Doha
mwaka huu ulieleza wazi mashaka yake juu ya athari ya ujenzi wa bwawa
hilo katika hifadhi.
Katika
mikutano yote hiyo ilikubalika kwamba mamlaka zinaozohusika nchini
kutofanya shughuli zozote za maendeleo ndani na kwenye mipaka ya hifadhi
bila kupata kibali cha WHC kwa mujibu wa kifungu 172 cha makubaliano.
Aidha
kamati hiyo iliitaka mamlaka zinazohusika kutekeleza ushauri uliotolewa
na kamati ya pamoja kati ya WHC na Muungano wa ushirikiano wa hifadhi
ya asili (IUCN) wa kutengenezwa kwa mkakati kabambe wa menejimenti ya
Ekolojia ya Selous.
Aidha
inatakiwa kutayarisha menejimenti hiyo kwa kuweka mipaka katika eneo la
urithi wa dunia na kuonesha maeneo ambayo yanastahili kuingizwa katika
hifadhi.
Pia
kufafanua mradi wa Stiegler’s Gorge, hatua iliyofikiwa hasa katika
maamuzi na kuhakikisha kwamba ufahamu kuhusu athari, gharama, manufaa na
namna inavyofaa au kutofaa na pia kuwa na mpango mbadala kama
haikuwezekana.
Mambo
yote hayo yanatakiwa kuzingatia umuhimu wa eneo hilo kwa jamii ya dunia
na hivyo kuangalia vigezo vyote vya maeneo ya urithi .
Katika
maamuzi hayo pia Kamati ya Urithi ilifurahishwa na nia ya mamlaka
husika za Tanzania kuendesha utafiti huo kwa mujibu wa makabaliano na
vigezo stahiki ili kuelewa athari zake katika hifadhi hiyo ambayo ni
urithi wa kimataifa, korido za mapito ya wanyama na nini kitatokea kwa
korido la Selous-Niassa Corridor.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, kamati hiyo ya Urithi wa Dunia (WHC) ilitarajia kupata taarifa za awali Februari Mosi mwakani.
Aidha
taarifa hiyo ilitakiwa kuwa na muhtasari wa hatua mbalimbali
zinazchukuliwa na muda wake kuhusiana na hifadhi ya Selou kujiondoa
katika urithi wa dunia ulio katika hatari ya kutoweka.
Imeelezwa kuwa taarifa hiyo ndiyo itakuwa msingi wa majadiliano katika mkutano ujao wa WHC wa 39 utakaofanyika Bonn Ujerumani.
Aidha
taarifa hiyo imesema kutokana na vitu vyote kutokuwa bado kufanyika
msimamo wa UNESCO unabaki kama ulivyo, kwamba hakuna makubaliano yoyote
yaliyofikiwa na kinyume na hapo ni kukiuka makubaliano.
Post a Comment