Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema
halitawaonea haya wale wote watakaosababisha kwa namna moja ama nyingine
kuharibika tena kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kurudiwa
kesho katika baadhi ya maeneo
Jumla ya mitaa 89 kutoka wilaya tatu za mkoa wa
Dar es Salaam, zinatarajiwa kufanya uchaguzi huo wa marudio kutokana na
kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa
Kanda Maalumu, jijini hapa, Kamanda Suleiman Kova, anasema wamejipanga
kila eneo kuhakikisha kuwa shughuli ya upigaji kura inafanyika kwa
Amani.
“vikosi vyetu viko salama vimejiandaa kukabiliana
na fujo zozote zitakazoweza kujitokeza, naomba nieleweke kuwa polisi
haitakuwa tayari kuwavumilia wale wote watakaosababisha vurugu,
tunawachukulia hatua za kisheria,”amesema Kamishna Kova.
Kamishna Kova anasema wametoa tahadhari kwa
wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa wakati wa
zoezi hilo ili wasije wakajikuta wanaingia kwenye mgogoro bila sababu
yeyote.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana,
alisema polisi wamejipanga vyema kuhakiki uchaguzi huo unaenda kwa
amani na utulivu kama ulivyopangwa.
“Kutakuwa na askari waliovaa sare nadhifu, na
askari wa kiraia ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wakati
wote amani inatawala katika vituo vya kupigia ,“ alisema Kamishna Kova.
Moja ya kasoro zilizopelekea kutofanya uchaguzi
katika baadhi ya vituo ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa
uenyekiti na wajumbe.
Manispaa ya Temeke ina mitaa 10, Kinondoni 16 na Ilala 63 .
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa manispaa ya
Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, ameingia kwenye mvutano mkubwa na
Chama cha Wananchi (CUF), juu ya uamuzi wake wa kutaka uchaguzi urudiwe
katika mtaa wa Mwinyimkuu ambayo inadaiwa chama hicho kilishinda
Post a Comment