Dar es Salaam. Kesi ya kupinga maazimio ya Bunge iliyokuwa ianze
kusikilizwa leo imeahirishwa hadi siku ya kufunga mwaka Desemba 31,
2014.
Wiki iliyopita za kampuni za IPTL na Pan Africa
Power Solutions (T) Limited (PAP) kwa kushirikiana na Harbinder Sighn
Sethi zilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la
muda la utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta
Escrow.
Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu
ambao ni Augustina Mwarija, Gadi Mjemas na Stella Mugasha jana ilipaswa
kuanza kusikilizwa lakini iliahirishwa baada ya mawakili wa upende wa
Jamhuri kuomba ahirisho ili waweze kujipanga.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju
aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa madai kuwa wao
walichelewa kupata maombi ya kampuni hizo hivyo walishindwa kuyasoma na
kujibu.
Hivyo aliiomba mahakama kuiaihirisha kesi hiyo
jana ili waweze kusoma na leo wawasilishe majibu yao na kama upande wa
pili na wenyewe utakuwa na cha kujibu watajibu ili Desemba 31,2014
isikilizwe.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,majaji
wanaoisikiliza kesi hiyo walikubaliana na maelezo hayo na kuiahirisha
hadi siku hiyo ya Desemba 31,2014.
Post a Comment