Katika
Kikao cha Baraza hilo kilichoketi mjini hapa juzi kutathmini Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa, wajumbe hao walisema kuwa sababu kuu ya baadhi ya
maeneo kuchukuliwa na upinzani ni mbunge huyo, ambaye pia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wakati.
Walisema
kuwa kati ya vijiji 84 vilivyopo kwenye jimbo hilo, vijiji vinane
vimechukuliwa na upinzani wakati kati ya vitongoji 436, vitongoji 49
vimechukuliwa na upinzani.
“Hii ni kutokana na mbunge wetu kuwa na ahadi hewa na kukataa baadhi ya ahadi alizowahi kutoa mwenyewe,” walisema wajumbe.
Akisoma
maazimio ya kikao hicho, Mwenyekiti wa UVCCM Singida Vijijini, Shaban
Mang’ola alisema kuwa kutokana na hali hiyo wamempa mbunge huyo muda wa
siku 14 tu kuweza kufika Singida mara moja kuonana na jumuiya hiyo na
kutoa maelezo ya kuridhisha juu ya mustakabali wa ahadi zake.
Aidha,
maazimio hayo yanasema kuwa iwapo mbunge huyo atashindwa kufanya hivyo
katika muda uliopangwa, UVCCM itaitisha mkutano mkuu wa vijana wa jimbo
na kutoa maamuzi watakayaona yanafaa.
Waziri
Nyalandu anadaiwa kuhamasisha na kuahidi kuwapatia mikopo vijana zaidi
ya 9,000 wa jimbo hilo, ahadi ambayo hajatimiza hadi hivi sasa. Wajumbe
walidai kuwa kila kijana aliyetaka kuchukua mkopo aliingia gharama ya Sh
8,000. Pia anadaiwa kuitisha ligi ya mpira wa miguu na kuahidi
kuwapatia zawadi washindi lakini baadaye akaikana ligi hiyo.
Aidha,
mbunge huyo anadaiwa kuwatukana hadharani baadhi ya wapiga kura wake
jambo, ambalo baraza hilo limekiita kuwa ni dharau kwa jumuiya ya umoja
huo.
Hata
hivyo, Nyalandu akizungumza kwa simu na Mpekuzi alisema taarifa
hizo hazina ukweli wowote na kwamba kuna watu walilipwa fedha kwa ajili
ya kumchafua na kukichafua chama.
“Habari
hizi ni za kuchafuana tu na uongo. Kuna watu walilipwa na Mwenyekiti huyo
wa UVCCM anajua, kisha wakaitisha mkutano kinyume na utaratibu pamoja
na waandishi wa habari, wakachaguliwa vijana watano ili kusema hayo
waliyosema. Kwenye Jimbo langu, CCM imefanya vizuri sana na huo ndio
ukweli,” alisema.
Nyalandu
ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii alisema katika jimbo lake
hilo la Singida Kaskazini, CCM imeshinda vijiji 179 na kushindwa katika
vijiji vinane na kuongeza kuwa huo ndio ukweli halisi na kuhoji kuwa kwa
idadi hiyo ya ushindi kweli CCM imeshindwa?
Kwa
mujibu wa Nyalandu, leo Kamati ya Siasa ya Wilaya inakutana katika
mkutano wa dharura ambapo watajadiliana kuhusu mwenyekiti huyo
anayedaiwa kuhongwa fedha na kufanya mkutano huo wa vijana usiokuwa
rasmi na kwamba moja ya hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa dhidi ya
Mang’ola ni kusimamishwa na chama.
“Ni
watu wenye nia mbaya tu wameamua kuitisha mkutano kinyume cha Sheria.
Lakini Kamati ya siasa ya wilaya inaitisha mkutano wa dharura na kuna
tamko litatolewa kuhusiana na mwenyekiti huyo, kwa sababu inajulikana
kabisa kwamba walipewa hongo kutoa taarifa hizo za uongo,”

Post a Comment