Baadhi
ya wananchi mkoani Kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani
waziri wa ardhi nyumba na makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine
walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakiongea na mwandishi mwetu, wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini
hatima ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. kikwete kwa
kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na
kumuuondoa waziri Tibaijuka na pia wamebaki na sintofahamu ambapo
wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha ya kumng’oa madarakani kiongozi
huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akaunti hiyo ya Tegeta Escrow au la.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo
katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kagera Hamimu
Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa wakati akiongea na
wazee wa jijini Dar es salaam kwa kumuondoa kiongozi huyo.
Kwa upande wake, katibu
wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika manispaa ya Bukoba
Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka
Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa lini
katika akaunti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho
na kwamba pesa hizo hazirudishi?.
Kwa
upande wake aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna
Tibaijuka amesema licha ya Rais kumuondoa katika nafasi yake
aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na
changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo
ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na
kwamba Pesa hizo alizopewa na Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na
alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti
ya Tegeta Escrow ndo maana hakutaka kujiuzulu.

Post a Comment