Hayo yalisemwa na Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Juma
Kaponda katika mkutano wa wadau wa elimu uliandaliwa kwa ajili ya
kutangaza matokeo ya darasa la saba.
Kaponda aliwataja walimu wakuu hao wanatoka katika shule za Mwiyendaje, Dk. Samwel Malecela na Segara wilayani Chamwino.
Wengine walioshushwa vyeo ni walimu nane kutoka
Wilaya ya Chemba ambao ni Makongoro, Konga, Hamia, Kubi, Ndoroboni,
Chiole, Kidoga na Chinyika.
Walimu wakuu wengine ni waliokubwa katika kadhia hiyo ni wa shule za Kongogo, Mkakatika na Bankororo Wilaya ya Bahi.
Katika wilaya ya Mpwapwa walioshushwa vyeo ni walimu wakuu wa shule za Luhundiwa na Idiro.
Aidha, Kaponda alisema mkoa wa Dodoma ushika
nafasi ya 21 kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka
huu wakati mwaka jana mkoa ulishika nafasi ya 23.
“Ufaulu huu umeufanya mkoa kubaki katika rangi
nyekundu za matokeo makubwa Sasa (BRN). Halmashauri zote zipo kwenye
rangi nyekundu,”alisema.
Hata hivyo, takwimu za ufaulu zinaonyesha hali
ya matumaini kwamba ufaulu umekuwa ukipanda kwa miaka yote miwili licha
ya ukweli kwamba kasi ya kupanda imekuwa ndogo,”alisema.
Kwa mujibu wa takwimu hizo kiwango cha ufaulu kwa
mwaka jana kilikuwa ni asilimia 38.2 (sawa na wanafunzi 15,053), ambapo
mwaka huu kimepanda na kufikia asilimia 45.3 (sawa na wanafunzi
16,672).
Post a Comment