Kiungo
wa Chelsea Cesc Fabregas amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya
Barclays Premier League kusaidia kupika magoli 15 (kutoka pasi zilizozaa
goli) katika misimu miwili tofauti.
Nyota
huyo wa zamani wa Arsenal amepika bao lake la 15 tangu ajiunge na
Chelsea akitokea Barcelona majira ya kiangazi wakati timu yake ikiifunga
Swansea 5-0 katika dimba la Liberty Stadium siku ya Jumamosi.
Fabregas
alianza kuweka rekodi msimu wa 2007-08 akiwa na Arsenal ambapo
alichangia magoli 17 wakati vijana wa Arsene Wenger wakimaliza katika
nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea na mabingwa Manchester United.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Hispania sasa anavizia rekodi ya Thierry Henry
aliyoweka miaka 12 iliyopita ya kutoa pasi zilizozaa magoli mara 20 kwa
Arsenal.
Post a Comment