Jeshi la wananchi wa Tanzania zaidi ya miatatu, wamefanikiwa
kudhibiti sehemu ya ardhi iliyobaki isiendelee kumezwa na maji ya bahari
kwa kutumia mawe na vifusi vya mchanga katika eneo la Msimbati lililopo
Mtwara vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio kanali wa
jeshi Saidi Nkambi anayesimamia oparesheni hiyo amesema zoezi hilo
linakwenda vizuri na tatizo linalosumbua kwa sasa ni mifuko kwa ajili ya
kujaza mchanga.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa Mtwara Ponsiano Nyama ametaka
wananchi wa mikoa ya Mtwara kuwa watulivu serikali inafanya kila juhudi
kuhakikisha dhoroba hiyo haileti madhara kwa mikoa ya Mtwara na Lindi,
huku muhandisi wa kiwanda kilichokaribu na bahari Peter John akiishukuru
serikali kwa hatua walizochukua
- ITV
Post a Comment