KUNA
watu wanaweza kupatwa na mshangao kwa kichwa cha habari hapo juu.
Watajikuta wakishangaa kwa sababu siku zote wamekuwa wakielewa kuwa
mapenzi ni hisia, kwa sababu yanamwendesha mtu vile anahisi. Leo nataka
kuwahakikishia kuwa kamwe, jambo hili siyo hisia, bali ni uhalisia!
Inaweza kuwa vigumu kuelewa mara moja maana yangu, lakini kuna mifano
rahisi na mifupi ninaweza kukupa ili uelewe maana yangu. Kunywa maji
wakati ukiwa na kiu siyo hisia, bali ni uhalisia, kutakiwa kuogelea
ukiwa ndani ya maji ni uhalisia, siyo hisia!
Ni kama vile ambavyo ukiwa umechoka na kuhitaji kujipumzisha kwa
kulala kidogo, zile siyo hisia, ni uhalisia, ingawa unaweza kusema
unajisikia vizuri kwa kujilaza. Hisia ni vitu vinavyotokana na tafsiri
pamoja na uzoefu, wakati uhalisia hauhitaji tafsiri, bali ni vitu
ambavyo vipo, vipo sawa na vinasomeka.
Kinachotokea ni kwamba sisi, kwa sababu ya kujiridhisha, tunatafsiri
mapenzi yetu na kuyafanya kuwa hisia. Mwanaume kumhitaji mwanamke siyo
suala la hisia, ni uhalisia, kama ilivyo kwa mwanamke anapomhitaji
mwanaume. Kama kuna mtu anaweza kubisha kuhusu hili, basi sitahitaji
kubishana naye kwa sababu ninajua sitaweza, isipokuwa nitaomba msaada
wako wewe msomaji, ni kweli unamhitaji mwenza wako kwa sababu ya hisia
zako au uhalisia wako?
Hisia zinabadilika kulingana na wakati, hakuna inayodumu kwa muda
mrefu. Unaweza ukampenda mtu kwa dhati leo, lakini kesho au mwezi ujao
ukamwondoa mawazoni. Labda kama hisia zako zitakuwa ni za kujiuliza ni
vipi kwa uzuri wote ule umebadilika haraka kiasi hicho!
Mwisho wa hisia, hugeuka kuwa kinyume chake. Kwa mfano, hisia zenye
mvuto mkubwa wa mapenzi, upendo na furaha, hugeuka kuwa chuki, hasira na
kutokuelewana. Hapo ni pale hisia zinapokuwa zimepoteza mwelekeo
unaotokana na maisha yanayoendelea wakati huo. Wakati hili linafanyika,
kwa maana ya hisia za mwenza mmoja kubadilika, haziondoi uhalisia wa
mahitaji yake ya jinsia nyingine katika maisha yake ya kimapenzi.
Kitu cha muhimu ninachotaka kubadilishana mawazo na wewe msomaji
wangu ni kwamba, katika mapenzi, tunao uhalisia wa mahitaji na tunazo
hisia za mahitaji. Mwanaume anaweza kuwa na uhalisia wa kuhitaji
kukutana na mwanamke, lakini hisia zinamlazimisha kumtafuta mwenye
kuendana na vigezo vyake.
Kwa mfano, Ben ni kijana anayependa wasichana wenye makalio makubwa, akiwapata, yupo tayari kupoteza kiasi chochote cha fedha alichonacho ilimradi awe nao wa aina hiyo.
Kwa mfano, Ben ni kijana anayependa wasichana wenye makalio makubwa, akiwapata, yupo tayari kupoteza kiasi chochote cha fedha alichonacho ilimradi awe nao wa aina hiyo.
Lakini kumbuka, ingawa anawahitaji wa namna hiyo, hiyo haina maana
kuwa hawezi kushiriki na wasichana wenye muonekano tofauti kwa muda wote
ambao wa vigezo vyake watakosekana. Hisia zitakaposhindwa kukamilika,
itabidi Ben awe katika uhalisia, wa kuhitaji mtu wa kuwa naye kwa muda
huo!
Lengo la mada hii ni kuwakumbusha kuwa katika maisha yetu ya
kimapenzi, tunavyo vitu vya lazima ambavyo tunatakiwa kuwa navyo na vipo
vitu ambavyo si vya lazima, lakini vinasaidia kulifanya penzi letu kuwa
katika sura tunayohitaji.
Kila mmoja angehitaji kuwa na mwenza wake na katika hilo, yapo
mahitaji ya msingi ambayo mume au mke ni lazima ayapate, bila kujali
mbwembwe. Vitu vya lazima vya kimapenzi vinazungumza kuhusu kutoka
kwenda matembezini siku za mwisho wa wiki, lakini havitaji eneo gani.
Hali ya maisha ya wapendanao inaamua kuhusu wapi kwa kwenda!
Kutoka kwenda matembezini ni jambo la lazima kwa wapendanao ili
kubadili upepo, lakini kwamba ni lazima kwenda katika hoteli kubwa, hizo
ni hisia zisizo na uhalisia!
Post a Comment