PAMOJA NA KUPIGWA VIBAO HADHARANI,HUH ASEMA HAMUACHI SHILOLE NG'O!

Hivi karibuni kwenye tamasha lililofanyika kwenye viwanja wa Leaders,Kinondoni jijini Dar,msanii wa Bongo Fleva,Shilole alimzaba vibao mpenzi wake,Nuh Mziwanda hadharani hali iliyozua tafrani hadi baadhi ya wasanii kuingilia kati.Habari zinasema pamoja na kuamuliwa asimpige mpenzi wake lakini bado Shilole alikuwa mkali baadaye msanii mwenzake,Steve Nyerere aliweza kumtuliza Shilole. 
Kupitia mtandao wa Instagram msanii Nuh Mziwanda alidhihirisha kuwa hawezi kumuacha mpenzi wake huyo pamoja na kwamba alimpiga vibao hadharani baada ya kuandika hivi…Mwanaume lijali aliekamilika ampigi mpenzi wake wala kurudishia kibao au kofi alilopigwa na mpenzi wake.naamini kwenye mapenzi ya kweli wivu lazima na kugombana kwenye mapenzi ni kama kwenda chooni ni swala la kawaida sana.aaaaaaaya mke wangu nimekup rukhsa nipige mpaka nikome.ila all i know its love dats it.Nawapenda Mashabiki wangu pamoja sana .#zimaTaa sie tayari….. Baadhi ya mashabiki wake walitoa maoni baada ya Nuh kuandika hivyo.. faithgabriella @asnathkasika hahahahahaha Xa Mahaba gan ayo ya kudundwa mbele za watu afu mtoto wa kiume xi uzoba uwo
kifimbo_cheza Wee Mtoto alie kwambia kugombana kwenye mapenzi ni kawaida, amekudanganya, MAPENZI HAYAUMI Na akupendae hakutakii maumivu ila Furaha, atapanda na kushuka kuhakikisha mpenzi wake upo na furaha, na sio kukudhalilisha mbele ya KADAMNASI.. Heshima ni Kitu cha bureeee, @mziwandanation


arnoldedge Na wew utakufa kwa kuendekeza njaa izo

janelicious4 Kwakweli ana kera sna hivi mwanaume mzima una simamamisha unapigwa mbele ya watu khaaaa kichefuchefu itabidi niombe ndimu maana umenikera sna @shilolekiuno nampenda ila kanifny nimchukie kbs hy sio maisha kuna watu maarufu kim kina flani (.....) watu wakubwa kushinda ht wewe uwa awafanyi hyo ujinga kbs sembuse wewe fala

pretynorah Kaka angu usiwe kama huyu bwege mtozene @kakytee

kishajeremiah @kijahmakoye nahisi hata wanavyoishi mziwanda ni full kupika, kuosha vyombo, kutandika, kudeki akiacha tu konde huyo ndo mwanaume


fatmamnwele Unatakiwa uhashimiwe km mwanaume hata km huna kitu asionyeshe mbele za watu mambo ya kuja kunyang'anywa funguo za gari na kuonyesha kwa watu kwamba kila kitu ni chake malizeni chumbani ugomvi wenu naimani wazazi wako wakisikia wanaumia

nletcher hahahhaaa..jaman!!mahaba nichape vibao nikalale..@mihohrey @zion_edu 3h

glowrymassawe07 @kipenzichao yan mamaake kwakweli anaumia sana bas tu atafanyaje,uko ni kujiabisha na kuaibisha familia yake pia...mi inaniuma ka nn...kwan mastaa wenzao wakiume wakowapi wamkanye uyo shishi??? ila pia kwan we nuhu kwamawazo yako yaliyoenea shishi wakwako pekeako??? fight kwa maisha yako yajayo we bado yunk...usiendekeze kulelewa na cyo mapenz yamekugandisha apo bali ni maisha ya burebure.....walllah utakufaga maskin ukimuendekeza uyo manzi tafta pesa na maisha yako uwe huru na amani
alikiba_diamond Kukupiga vibao hadharani hyo ni hatua ya mwisho katika ugomvi wa mausihano,,,,shishi anajaribu kuongea nå ww kwa vitendo,,,watu hawakushauri uachane nae,,watu wameguswa nå tukio hlo..chukua tahadhari kua makini nå huyo binti.... MIMI NI SHABIKI NINAEVUTIWA NÅ KAZI ZAKO SI UHUSIANO WAKO

Post a Comment

Previous Post Next Post