Hatimaye
nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu
ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa
ya soka.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye
majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa
nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo
na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya.
Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo
kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki
moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa
kumuangalia vizuri.
credit:Shaffdauda
Post a Comment