Aliyekuwa
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema uadilifu
unahitajika katika sekta ya Nishati na Madini pasiwepo na rushwa kwani hiyo ni
kuweza kusaidia watanzania masikini wanaongalia sekta hiyo kwa maendeleo ya
uchumi wao.
Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akikakabidhi ofisi kwa Waziri mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene,amesema lazima kuwepo na uzinagatiaji wa mikataba ili watanzania waweze kunufaika na rasilimali zao.
Source:michuzi Blog
Muhongo
amesema Simbachawene sio mtu wa tamaa siku zote alipokuwa Naibu wa Waziri wa
Nishati na Madini walikuwa wakiambiana juu ya kuwatumikia watanzania wengi na
sio mtu binafsi.
Amesema lazima tujenge uchumi imara kutokana na sekta hii ili watanzania waweze kukua kiuchumi kutokana na sekta ya madini inavyokua kwa kasi.
Muhongo amewataka waandishi kuelimisha watanzania kwa ajili ya ustawi wa taifa na sio mtu mmoja au ubinafis wa mtu.
Kwa upande wa Simbachawene amesema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika,kwani ofisi ya umma sio mali ya mtu.

Post a Comment