Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso),
imeiomba serikali kuidhinisha vyeti vya wa wahitimu wa elimu hiyo kama
moja ya dhamana ya kupata mikopo katika taasisi za fedha kama ilivyo
hati za nyumba.
Rai hiyo ilitolewa mbele ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, katika mkutano wa kuzungumzia suala la ukosefu wa ajira na mikopo kwa wanafunzi uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Tahliso, John Francis, alisema kutokana na matatizo hayo kuonekana kuwa sugu, wameamua kuiomba serikali kuidhinisha vyeti vya wahitimu wa elimu ya juu vitumike kupata mikopo kutoka katika mabenki kwa lengo la kujiajiri wenyewe.
Francis alisema endapo serikali itaruhusu hilo, itakuwa imetatua tatizo la ajira kwa wahitimu kujiajiri wenyewe.
"Tumeiomba serikali iidhinishe vyeti vya wahitimu wa elimu ya juu vitumike kama dhamana ya kupata mikopo. Lengo itusaidie katika kujikwamua na tatizo la ajira baada ya kuhitimu masomo," alisisitiza Francis.
Alisema kama ombi hilo litakubaliwa, litasaidia kuwakwamua wanafunzi wengi wanaohitimu masomo hapa nchini na kukosa ajira na hatimaye kuzagaa mijini.
Aidha, Tahliso ilijadili pia suala la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambayo imeonekana kuwa na tatizo na kusababisha wanafunzi kugoma.
Francis alisema tayari wamewasilisha suala hilo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kuahidi kuwa watalifanyia kazi.
Naye Dk. Mahanga aliwataka wanafunzi hao kuwa na subira kutokana na kwamba tatizo la ajira haliko Tanzania tu bali nchi nyingi duniani.
Hata hivyo, alisema serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya Tahliso kuona namna ya kuyatatua

Post a Comment