Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wamedhulumiwa zaidi ya Shilingi bilioni 50 za mauzo ya zao hilo , Bunge limeelezwa.
Zambi alisema zao hilo pamoja na kusaidia kukabiliana na changamoto
ya ukosefu wa ajira nchini ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya pato la
taifa ambapo mwaka jana, liliongoza kuleta fedha za kigeni
Hayo yalielezwa na Zitto Kabwe (Chadema Kigoma Kaskazini),
alipouliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
akitaka tamko la serikali kuhusu upotevu huo wa fedha za wakulima wa
tumbaku mkoani Tabora.
Alisema wakulima wamedhulumiwa Dola milioni 28 sawa na Shilingi
bilioni 50 kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG).
Licha ya fedha za wakulima hao mkoani Tabora, kupotea mwaka jana
hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali kukabiliana na
upotevu huo.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi
alikiri kwamba serikali inatambua upotevu wa fedha nyingi za wakulima
mkoani Tabora, akithibitishia kuwa taarifa hizo zilipofika wizarani na
hatua zilichukuliwa kwa kupeleka wakaguzi.
Alisema kwa kuzingatia taarifa ya CAG, suala hilo liliwasilishwa
ofisini kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na kwamba linaeandelea
kufanyiwa kazi, na lipo katika hatua tofauti za utekelezaji.
“Kilichobainika ni kwamba wizi huu unafanyika maeneo mbalimbali
nchini na unashirikisha baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na
watumishi wa benki wasio waadilifu,” alieleza Naibu Waziri Zambi.
Katika swali la msingi, Rukia Kassim Ahmed (Viti Maalum), alitaka
kufahamu ikiwa serikali imefanya utafiti wa kina juu ya faida na hasara
inayopatikana kwenye tumbaku.
Kadhalika alihoji endapo serikali ipo tayari kuwasaidia wakulima
wa zao hilo, kupata mbadala wa tumbaku ili kuepusha madhara kwa afya
zao.
Post a Comment