Jeshi la polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watu 96 wengi wao
wakiwa ni raia wa nchi jirani ya burundi, wanaotuhumiwa kujihusisha na
ujangili kwenye hifadhi ya taifa ya katavi ikiwa ni pamoja na mapori
mbalimbali ya akiba (game reserve) mkoani katavi, na kukutwa na silaha
nne pamoja na risasi 118 na radio call kwa ajili ya mawasiliano.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi mrakibu mwandamizi wa
polisi FOCUS MALENGO, akiongea mjini mpanda amesema mafanikio hayo
yanatokana na operesheni maalumu iliyofanywa na askari wa jeshi hilo la
polisi kutoka mikoa ya Dar na Tanga, kwa ushirikiano na vyombo vingine
vya ulinzi na usalama, ikiwa na lengo la kupambana na vitendo vya
ujangili vinavyoendelea mkoani humo vinavyohatarisha uwepo wa baadhi ya
wanyama na raslimali nyingine ambazo ni vivutio vya utalii.
Hata hivyo kaimu kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani katavi
hakuwa tayari kufafanua juu ya baadhi ya watuhumiwa hao ambao
wamehamishwa kutoka mkoani katavi, mahali walikohamishiwa na idadi yao,
ingawaje inaaminika kuwa ni raia wa nchi ya jirani ya burundi, ambao
wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ujangili, na kuishi katikati ya
mapori yaliyoko mkoani katavi.
Post a Comment