WAZAZI WA MANAIKI WAMTOLEA NJE WOLPER

Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga,amesema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwa sababu wazazi wake wamemtolee nje ishu ya kwenda kumposa staa wa kike Bongo, Jacqueline Wolper.

Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga akiwa na Jacqueline Wolper.

Akizungumza kwa masikitiko, Manaiki alisema kuwa hivi karibuni alifunga safari na kwenda kijijini kwao Mbeya kwa ajili ya kuwaeleza wazazi wake nia yake ya kumuoa Wolper lakini imekuwa tofauti kwani wamemwambia kama anataka kuoa msichana atatoka nyumbani kwao.

“Yaani nimeamini kabisa mbio za sakafuni huishia ukingoni, sikujua kama wazazi wangu watanikata maini kwa kuwa nilijua wazi hawatakuwa na kipingamizi lakini wameniambia kuwa lazima nioe nyumbani,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post