Bomu
limelipuka kazkazini mwa Nigeria nje ya uwanja mmoja wa soka ambapo
rais Goodluck Johnathan alikuwa amehutubia mkutano wa kampeni za
uchaguzi.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuko huo ulitokea katika
eneo moja la kuegesha magari dakika chache tu baada ya rais huyo
kuondoka katika uwanja huo uliopo mji wa Gome.
Bwana Johnathan anafanya
kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi unaotarajiwa tarehe
14 mwezi Februari,lakini anakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama
kutoka kwa kundi la Boko Haram huku kundi hilo likiimarisha mashambulizi
yake.
Siku ya jumapili watu watano waliuawa na bomu huko Gombe
- BBC
Post a Comment