Msanii mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koletha’
MUIGIZAJI wa
filamu Bongo, Koletha Raymond ‘Coletha’ amejikuta akiwa hana kitu baada
ya kukombwa shilingi milioni moja na nusu, nguo zake zaidi ya ishirini
na vifaa vya kuchukulia video wakati wakiwa lokesheni maeneo ya Mtoni
Kijichi, jijini Dar.
Coletha Raymond ‘Koleta’.
Akizungumza na Uwazi, Coletha alisema aliitwa lokesheni kucheza filamu
ya Mkono wa Kushoto ambapo alikuwa tayari ameshapewa pesa ya utangulizi
shilingi milioni moja na nusu.
“Niliziweka pesa kwenye begi langu la nguo. Tulifika eneo ambalo gari
yetu haikuweza kupita kutokana na kuwekwa magogo njiani. Kwakuwa
tulihakikishiwa usalama ikabidi tuache gari na vitu vyetu kwa muda na
kusogea eneo la mbele kidogo. Kitendo cha kumaliza na kurudi tukakuta
milango ya gari ipo wazi na vitu vyetu vyote havipo,” alisema Coletha
Post a Comment