Beyoncé Lawamani Kwa Kufuru Aliyoifanya Katika Video Ya Wimbo “Feeling Myself”

Mrs Carter aka Blue Ivy Mama yupo lawamani. Ipo hivi; kama umeiona video mpya ya wimbo Feeling Myself ambao ni ushirikiano wa Beyonce na Nicki Minaj, utaona sehemu fulani Beyonce akimwaga champagne kwenye hot tub.
Kwa bahati nzuri au mbaya ile sio champagne ya kawaida tu kama zile ambazo mtu yeyote anaweza kununua kutoka Dollar Store. Ni Ace Of Spades ambayo inagharimu Dola za Kimarekani $20,000. Kwa bei ya leo ya masoko ya fedha duniani, hiyo ni sawa na shilingi za kitanzania takribani milioni 41!
Kwa mujibu wa mtandao wa Gossip Cop, imeshakuwa nongwa. Mashabiki wamefumuka mitandaoni wakiponda “kufuru” hiyo kwa kusema chupa hiyo moja (kwa maana ya fedha) ingeweza kutumika kuwasaidia watu kibao. Wanasema pesa hizo zingeweza kumsaidia mtu masikini kupata mlo wake wa mchana nk.
Lakini kuna ambao wamejitokeza na kumkingia kifua Beyonce kwa kusema ameshafanya mengi ya kusaidia jamii na hivyo anaweza “kujiachia” kiaina. Wewe unasemaje? Unadhani ni sawa kwa Beyonce kufanya kufuru hiyo au? Cheki video hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post